Wednesday, September 5, 2018

Yanga na Simba kushuka Dimbani weekendi hii kujipima nguvu Taifa


Baada ya kuhairisha safari ya kuelekea Kigoma kucheza na Singida United Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya African Lyon siku ya Jumapili ya Septemba 9 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni  na kuonyeshwa moja kwa moja na Azam TV Viingilio vya mechi hiyo,vitakuwa ni shilingi 3000 kwa mzunguko, 5000 kwa VIP B na 10000 kwa VIPA A.


Yanga wanacheza na African Lyon wakiwa wamecheza mchezo mmoja tu wa ligi dhidi ya MTIBWA sugar waliowafunga magoli 2-1 na mchezo huu ni wa maandalizi ya muendelezo wa ligi kuu mara baada ya ligi kusimama kwa muda .Wakati huohuo watani zao wa jadi Simba, nao watakuwa Uwanjani hapo Jumamosi ya wiki hii kucheza mechi ya kirafiki na AFC leopards ya Kenya majira ya saa 1 jioni.

Na viingilio vya mchezo huo kuwa ni VIP A ni sh 15,000 VIP B na C sh 10,000 na mzunguko sh 5000.
Afisa habari wa Simba Haji Manara ameandika katika ukurasa wake wa instagram kuwa mashabiki wataitazama mechi ya Stars dhidi ya ‘The Cranes’ kupitia Screen kubwa iliyopo uwanjani hapo kabla ya mchezo huo wa kirafiki.
SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: