Tuesday, September 18, 2018

Yanga kuwakabili Coastal Union,Alliance dimbani leoLigi Kuu Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa michezo sita kupigwa kunako viwanja Sita tofauti ambapo macho ya wapenda soka wengi yataelekezwa  jijini Dar es salaam Yanga ikiumana ana Coastal Union.

Mechi hiyo ya  mabingwa wa kihistoria katika ligi, Yanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga utapigwa uwanja wa Taifa kuanzia saa 1 jioni.

Kuelekea mechi hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya kipute hicho dhidi ya wagosi wa kaya.

Kwa upande wa vijana wa Costal union kupitia kwa msemaji wa timu hiyo Hafidhi Kido alipozungumza na FAMARA NEWS amesema wamejipanga vizuri na kuhusu Mchezaji wao Alikiba kucheza ni mipango ya Benchi la ufundi likiongozwa na Mwalimu Juma Mgunda.

Aidha, katika Uwanja wa Samora huko Iringa, Lipuli itakuwa inaikaribisha Alliance FC ya Mwanza mechi itakayoanza majira ya saa 8 mchanan kwa saa za Afrika Mashariki.

Pia kunako dimba la Mwadui Complex wenyeji ambao ni Mwadui FC watakuwa wanacheza dhidi ya JKT Tanzania kuanzia saa 10 kamili jioni.

Mechi nyingine za majira hay hayo ya saa kumi kamili ni ile ya Biashara United wakiwakaribisha wanalambalamba Azam FC wakati “wagonga nyundo wa jiji la mbeya” Mbeya City wakiumana na  Ruvu Shooting kutoka kule mkoani Pwani.

Mchezo wa meingine hii  Ndanda FC  baada ya kuambulia alama moja mbele ya Simba watawakaribisha Mtibwa Sugar ambayo nayo iliambulia alama moja dhidi ya Lipuli kule Iringa.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: