Friday, September 7, 2018

Wimbo mpya wa Sema na Yesu wake Happy Mlinga kuachia rasmi.


Hatimaye Mwimbaji Staa wa Muziki wa Injili kutoka Dar es Salaam Tanzania Happy Mlinga kesho September 8 ataachia wimbo wake mpya audio Youtube ili kuendelea kuwapa mashabiki na wapenzi wake raha ya kusikiliza muziki mzuri wenye upako na unaogusa mioyo.

Akizungumza na Mtandao wa Famara News, alisema kuwa ameamua kufanya kazi kubwa ambao itakwenda mbali kimataifa na lengo likiwa kumtukuza Mungu aliyempa pumzi na sauti ya kuimba.

''Nimekamalisha wimbo wangu mpya uitwao Sema na Yesu, ni wimbo mzuri sana na ambao kila atakayeusiki lazima aguswe na kubarikiwa kwa ujumbe uliyomo ndani humo, hivyo niwaombe mashabiki wangu wote kesho September nane saa tano na dakika hamsini na tisa utakuwa Youtube'' alisema.

Wimbo huo utaachiwa kesho Youtube ya Happy Mlinga na Famara Tv ili kila mtu apate nafasi ya kuusikiliza ili aweze kujengwa na kuinuliwa upya kiroho na kimwili.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: