Sunday, September 2, 2018

Waziri Kangi Lugola atoa onyo kwa Askari Polisi nchini- Famara Media Group.

NA OSCAR MIHAYO,MWANZA
WAZIRI wa mambo ya ndani ya Nchi,  Kangi Lugola, ametoa onyo kwa Askali Polisi nchini kutotumia nguvu zinazoumiza raia.
Amesema kufuatia uwepo wa matukio ya wananchi kupata ulemevu na wengine kufia himaya ya Jeshi hilo na kuanza kuzua mjadala mkubwa kwenye jamii halikubaliki.
Lugola ametoa kauli hiyo jana jijini hapa alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari , ikiwa na kuwamewataka Askari Polisi kote nchini kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za Jeshi la Polisi sura namba 322 na kanuni za kudumu za Jeshi la Polisi.
“Askari Polisi watumie nguvu kulingana na mazingira yaliyopo eneo husika ili kuepuka kutumia nguvu za ziada isipokuwa itakapobidi na kwa mjibu wa sheria kama wanavyoimba kwenye wimbo wao kwani hakuna mtu aliyejuu ya sheria,” alisema Lugola.
Waziri Lugola pia amelaani tukio lililofanywa na na Mgambo katika Jiji la Dar es Salaam, akiliita la kihuni, kishenzi na kinyama na kuongeza kuwa halipaswi kufumbiwa macho na wapenda amani haki za binadamu na wananchi wote kwa ujumla.
Kauli hiyo imekuja siku moja mara baada ya tukio la askari mgambo watatu kuonekana na kweye kipande ha video wakimpiga raia Robson Olotto na kuzuioa taharuki kwenye mitandao ya kijamii na wapenda amani kote nchini.
“Natumia fursa hii kuwakumbusha tena mgambo wote kuwa makini katika utekelezeji wa maagizo wanayopewa ikiwa na kufuata sheria na kanuni na taratibu za nchi,” alisema mbunge huyo wa jimbo la Mwibara.
Kufuatia mgambo hao kukiuka kanuni na taratibu kwa kutumia nguvu pasipo husika  amewataka Halmashauri na Majiji kuona namna ya kuajiri askari wa wasaidizi (Auxiliary Polisi)  ili kuepuka tabia za uvunjifu wa haki za binadamu.
Lugola alieleza askari wasaidizi wapo kwa ajili ya mujibu wa sheria za Polisi sura namba 322 na wamepatiwa mafunzo na namna ya kuwa na nidhamu na wanawajibika kwa Inspekta Jenalali wa Polisi.
Alisema Nchii hipo chini ya utawala wa sheria ni vyema kila mtu atekeleza majukumu yake kwa kufuata taratibu na kanuni za nchi.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: