Monday, September 10, 2018

WANAUME WASISITIZWA JUU YA KUPIMA VVU. Na WAMJW-NACHINGWEA. 

WANAUME Mkoani Lindi Wilaya ya Nachingwea wamesisitizwa juu ya masuala ya kupima virusi vya Ukimwi ili kujua hali ya maambukizi kwa wakazi wa mkoa huo. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kilele cha kampeni ya Furaha yangu leo katika Tarafa ya Naipanga wilaya ya Nachingwea Mkoani humo. 

"Kwa sasa Serikali imejipanga kutomomeza maambukizi ya Ukimwi kwani kila takayepima na kugundulika ana maambukizi ataanza kutumia dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi mara moja ili kufikia lengo la 909090 ifikapo mwaka 2020" alisema Dkt. Ndugulile. 

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa bado idadi ya wanaume wanaojitokeza kupima VVU ni ndogo hivyo kuwataka wanawake wawahimize waume na vijana wao wa kiume kujitokeza kutambu afya zao.

Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile aliutaka uongozi w Hospitali ya Wilaya ya Nchingwea kuboresha mazingira ya kutunzia dawa,  chanjo , damu na vitendanishi kwani bado havipo kwenye mpangilio mzuri wa kuhifadhi. 

"Kiukweli mazingira ya Hospitali sijayapenda hivyo nawapa onyo kwa mara ya mwisho na mchukue hatua haraka ya kuboresha mazingira yenu na hali ya utoaji huduma na kuhakikisha kila mtumishi awe Daktari au Muuguzi kujaza taarifa za mgonjwa kila anapomuhudumia kabla ya Serikali kuchukua hatua stahiki dhidi yenu" alisisitiza Dkt. Ndugulile. 

Aidha Dkt. Ndugulile alibainisha kuwa Serikali imeipatia Wilaya hiyo kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Hospitali ya Wilaya hiyo ili kuweza kutoa huduma bora za Afya kwa wananchi wa Wilaya hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mhe. Rukia Mwango amesema kuwa anayo furaha kusikia hali ya  maambukizi katika mkoa wao umepungua kutoka asilimia 3. 7 mpaka kufikia asilimia 0. 3. 

Aidha Bi. Mwango amesema kuwa wananachingwea hawana budi kujitokeza kupima VVU kwani maendeleo yao yataletwa na wananchi wenye afya njema na kujitambua kwa uchumi wa Nachingwea. SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: