Monday, September 3, 2018

Wanalambalamba Azam fc kuumana na Arusha united kesho chamaziKLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inatarajia kucheza Mchezo wa kirafiki dhidi ya Arusha United ya mkoani Arusha kwa lengo la kuiweka timu hiyo vizuri kwa ajili ya muendelezo wa ligi kuu Tanzania bara (TPL).

Benchi la ufundi la Azam FC limeamua kufanya hivyo ili kuwaweka kwenye ushindani wachezaji ambao hawajacheza mechi mbili za awali za Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), ambayo imesimama kwa muda kwa baadhi ya timu.

Ligi hiyo imesimama kupisha mechi ya kufuzu Mataifa ya Afrika mwakani nchini Cameroon kati ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Uganda ‘The Cranes’ itakayofanyika jijini Kampala Septemba 8 mwaka huu.

Mkuu wa idara ya habari wa Azam Jaffary Iddi Mganga amesema,anawaomba washabiki wajitokeze kwa wingi hapo kesho kushuhudia mtanange huo dhidi ya  Arusha united ya mkoani Arusha.

Kwa upande wake mkurugenzi wa klabu ya Arusha United Saad Kawemba amesema anaamini michezo hii ya kirafiki itakuwa na tija kwao mara baada ya kucheza na simba na kufungwa magoli 2-1 na kuwaomba mashabiki wa soka kanda ya kaskazini wawape sapoti ya kutosha.

Mchezo huo wa kirafiki utafanyika katika uwanja wa azam complex Chamazi nje kidogo ya jiji la dar es salaam majira ya saa kumi na mbili kamili jioni.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: