Friday, September 7, 2018

Walioshinda tuzo ya soka ligi kuu Uingereza kwa mwezi August 2018.Lucas Moura Mchezaji bora wa mwezi
Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham, Lucas Moura, baada ya kuiadhibu Manchester United kwa kufunga goli mbili peke yake kwenye ushindi wa 3-0 ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa Mwezi August katika ligi kuu ya uingereza.
Lucas Moura mchezaji wa zamani wa PSG amefunga magoli matatu hadi sasa akiwa na msimu mzuri saana.
Moura amewashinda wachezaji hawa
Goli bora la mwezi
Mshambuliaji wa klabu ya Fulham, Jean Michael Seri ametwaa tuzo ya goli bora la Mwezi August, katika ligi kuu ya uingereza .
Seri, alifunga bao katika mchezo wa ligi kuu England dhidi ya Burnley, hapo Mwezi August 26 mwaka huu.
Seri mwenye umri wa miaka 27 alimfunga goli hilo goli kipa wa zamani wa Man city Joe hart katika mchezo wake wa kwanza.
Seri amewashinda hawa na kutwaa tuzo ya goli bora la mwezi pale uingereza
Kocha bora wa mwezi
Kocha wa klabu ya Watford, Javi Gracia, ametwaa tuzo ya kocha bora wa Mwezi August, katika ligi kuu nchini Uingereza.
Watford Wameshinda michezo yao minne chini ya kocha huyo na kuungana na klabu za Livepool na Chelsea ambazo nazo zimeshinda michezo yote minne hadi sasa.
Watford walifungua ligi kwa ushindi wa 2-0 nyumbani dhidi ya Brighton & Hove Albion kabla ya kushinda  3-1 dhidi ya  Burnley na kuifunga  Crystal Palace 2-1 wakiwa nyumbani kabla ya kuifunga spurs magoli 2-1 pia .
Tuzo hii ni ya pili kwa kocha wa Watford kuishinda mara baada ya Quique Sanchez Flores kufanya hivyo mwezi December 2015.
Javi Gracia amewashinda Jurgen Klopp wa Liverpool ,  Mauricio Pochettino wa Spurs' na  Maurizio Sarri wa Chelsea .


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: