Sunday, September 2, 2018

Wakristo wote wakumbushwa kuwa nuru ya ulimwengu katika matendo yao.

Fabian Fanuel @FMG,
Kiloleli- Mwanza.

Wakristo kote duniani wakumbushwa kuwa nuru ya dunia ili waweze kuangaza katika kila wanalolifanya katika kutumkuza Mungu hapa duniani.

Wito huo umetolewa leo na Mzee wa Kanisa hilo Bi Lydia Kisanji wakati akihibiri katika ibada ya jumapili katika kanisa la EAGT Kiloleli, kanisa linalochungwa na Mchungaji Daktari Jacob Mutashi.

Bi Kisanji alisema kuwa kila mkristo anapaswa kuwa na matendo yanayoangaza kama nuru ilivyo na kuacha matendo maovu yanayoondoa utukufu wa Mungu katika maisha yao.

Alisema kuwa duniani kuna mambo mengi ambayo sio mazuri hivyo kila mkristo popote alipo anatakiwa kujisimamia na kumtegemea Mungu na kuepuka kufanya  mambo  yasiyofaa ambayo yanaweza kuondoa utakufu wa Mungu kwao.

Ameongeza kuwa kila mkristo ana wajibu wa kuhakikisha nuru ya taa yake inaangaza zaidi huku akimpinga shetani na mambo ambayo yanaweza kuondoa tabia ya kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli.


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: