Wednesday, September 19, 2018

VIDEO-Messi akipiga tatu, Barca ikitakata ligi ya mabingwa ulaya



Klabu ya FC Barcelona ikiongozwa na Nyota wao Lionel Messi aliyefunga  mabao matatu hapo jana imeibuka na ushindi mnono wa magoli 4-0 dhidi ya PSV Eindhoven katika mchezo wao wa kwanza wa ligi ya mabingwa ulaya.

Mchezo huo wa kundi B umepigwa katika Uwanja wa Camp Noun a magoli hayo matatu ya Messi yamefungwa dakika za 31, 77 na 87 huku goli lingine la Barca likifungwa na Ousmane Dembele dakika ya 74.

Hata hivyo Barca ilimaliza pungufu katika mchezo huo mara  baada ya   beki wake Samuel Umtiti kuonyeshwa kadi nyekundu dk ya 79 ya mchezo.

Magoli yote ya Barcelona tazama hapa….



SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: