Wednesday, September 12, 2018

VIDEO-Hispania ilivyowachapa makaimu bingwa wa kombe la dunia 6-0


Timu ya taifa ya Hispania imeipa kipigo cha mbwa mwizi timu ya Croatia kwa kuifunga mabao 6-0 katika mchezo wa michuano ya Ulaya kwa timu za taifa usiku wa jana.
Hispania inayonolewa na Luis Enrique ambaye ni kocha wa zamani wa FC Barcelona  ilifunga mabao matatu katika kila kipindi huku mshambuliaji wa Real Madrid Marco Asensio aking’ara.
Asensio amehusika katika mabao matano kati ya sita huku akifunga moja akisaidia matatu huku shuti lake likimgonga mlinda Lovre Kalinic na kuingia wavuni.
Hispania ilitawala mchezo muda wote wakati Croatia ambao walipoteza mchezo wa fainali wa kombe la dunia dhidi ya Ufaransa Julai mwaka huu wakishindwa kupiga hata kona moja huku wapinzani wao wakipiga nane.
Mabao ya Hispania yalifungwa na Saul Niguez, Asensio, Kalinic, Rodrigo, Sergio Ramos na Isco.
Mlinda mlango David De Gea alikuwa hana kazi kubwa ya kufanya kutokana na muda wote Hispania kumiliki mpira.
Katika mchezo wa kwanza Hispania ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Uingereza.
Michuano hiyo itaendelea tena mwezi Oktoba.

SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: