Monday, September 3, 2018

VIDEO-Bodi ya ligi yashusha rungu kwa Mbao FC,Coastal Union na waamuzi walioborongaKamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi iliyokutana Septemba mosi imetoa adhabu kwa timu mbalimbali za ligi kuu kutokana na matukio yalijitokeza katika michezo ya  mzunguko wa kwanza na wapili wa ligi kuu soka Tanzania bara(TPL).
Ofisa Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura  amesema mchezo wa Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar uliofanyika katika uwanja wa Taifa timu hizo zimepewa onyo kali baada ya kushindwa kuwasilisha majina ya wachezaji watakao tumika katika kikao kabla ya mchezo (Pre match meeting).

Katika mchezo huo mwamuzi Silvester Mwanga amepewa onyo kali kwa kushindwa kutafsiri sheria wakati kamishna wa mchezo Juma Chopanga akifungiwa miezi mitatu.
Zaidi kuhusu maamuzi ya  Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi  tazama hapa…..
SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: