Monday, September 10, 2018

Ujio wa Vilabu vya kenya Nchini wazua kizaazaa ,TF wakumbusha jamboShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  limesisitiza vilabu,wadau  na wanachama wa shirikisho hilo kutokukualika vilabu kutoka nje ya nchi kwa ajili ya michezo ya kirafiki bila kibali kutoka TFF na kufuata taratibu za shirikisho la mpira duniani FIFA.

Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Salum Madadi, ameyasema hayo leo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari na kusema wamefikia maamuzi ya kuvikumbusha vilabu mara Baada ya vilabu vya Simba na Biashara united kuvialika vilabu vya nje bila kufuata utaratibu.

Klabu ya Simba iliwaalika AFC Leopards ya Kenya kuja nchini kucheza huku Biashara united wakiwaalika Sonny Sugar nayo kutoka Kenya kuja kucheza mchezo maalumu wa kuzindua uwanja wao wa Karume kule mkoani Mara.

Madadi amesema ili michezo hiyo ya kimataifa ya kirafiki ichezwe ni lazima taaribu hizo zifuatwe.

"Ni lazima ruhusa itolewe na chama au shirikisho la mpira wa miguu la nchi husika kwa klabu husika inayotaka kwenda nje ya nchi yake kucheza mechi ya kirafiki " alisema Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Salum Madadi

Madadi amesema walishapata shida hiyo wakati timu ya wanawake ya Twiga stars ilipoalikwa Cameroon kwa mchezo mmoja wakanogewa na kucheza mchezo mwingine na TFF ikapigwa faini.SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: