Wednesday, September 5, 2018

Ubora wa kikosi timu ya soka la ufukweni Tanzania waendelea kuongezeka.

Nahodha wa timu ya taifa ya soka la ufukweni Juma Ibrahim amezungumzia juu ya program yao na ubora wa kikosi chao kuelekea mchezo dhidi ya Afrika Kusini siku ya Jumapili kwenye fukwe za Coco.

"Maandalizi yetu ni mazuri chini ya makocha wetu Katwila, Adolf na Pawasa, wiki ya kwanza tulianza kwa mazoezi magumu, wiki ya pili mazoezi yakawa mepesi na sasa tunafanya mazoezi ya mbinu."

"Tumepata mechi za kirafiki tulicheza na Magereza halafu tukacheza wenyewe kwa wenyewe (Zanzibar na Bara), tupo vizuri kiujumla hakuna majeruhi na tupo tayari kwa mchezo."

"Mechi hii ni muhimu sana kwa sababu tukiitoa Afrika Kusini tunafuzu kwenda AFCON Misri, kwa hiyo mechi ni muhimu sana ukilinganisha na miaka miwili iliyopita ambapo tulitolewa na Misri pamoja na Ivory Coast. Kwenye ranking za FIFA Afrika Kusini wapo chini yetu kwa hiyo tumejiandaa kuhakikisha mwaka huu tunafuzu."

"Kikosi chetu kipo vizuri, tumeongezewa nguvu na wachezaji kutoka XI kama Musa Mgosi, Yahaya Tumbo na mimi ambaye nina uzoefu wa soka la ufukweni tangu mwaka 2015 lakini pia tuna wachezaji vijana."


Chanzo- Mkazuzu

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: