Wednesday, September 5, 2018

Timu ya Taifa ya soka la ufukweni yafuzu Fainali za Afrika kule Misri jioni yaleo yatoa dozi nzitoTimu ya Taifa ya Soka la Ufukweni ya Tanzania imepata mteremko na sasa imefuzu moja kwa moja kucheza Fainali za Africa zitakazofanyika nchini Misri. 

Timu ya Tanzania imefuzu kucheza Fainali hizo baada ya mpinzani wake Afrika Kusini kuwasilisha barua ya kujiondoa katika mashindano Hayo. 


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia ukurasa wao maalumu wa Instagram ni rasmi sasa timu hiyo imefuzu  Fainali hizo za Afrika zitakaofanyika Misri mwaka huu kuanzia Desemba 9-Desemba 14,2018 na kushirikisha nchi Nane.


Timu hiyo ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni leo imecheza mchezo wa kirafiki  dhidi ya magereza na kuibuka na ushindi wa magoli 16-3.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: