Saturday, September 1, 2018

TAMASHA | Jumapili 2 September 2018, Uwanja wa Jamhuri Morogoro moto kuwaka.


Lile tamasha kubwa ambalo lilikuwa linasubiriwa kwa hamu muda mrefu Mkoani Morogoro ambalo litafanyikia katika Uwanja wa Jamhuri maandalizi yake yamekamilika asilimia mia moja, huku akiwaasa wakazi wote wa mkoa huo kujitokeza kushiriki baraka hiyo kubwa. 

Akizungumza na Famara News Mratibu wa Tamasha hilo Pasta Tumaini Njole Sehaba amesema kila kitu kimekamilika kuelekea Jumapili kesho kwa tamasha hilo ambalo litakuwa na mambo mawili makubwa, kuadhimisha miaka kumi na tano yeye kuwepo kwenye huduma na kuzindua albam yake mpya ya video.

Amesema waimbaji mbalimbali kutoka maeneo yamekwisha kufika mjini Morogoro ili kuwasha moto wa Mungu kwenye Uwanja wa Jamhuri kesho, ambapo watoto watalipia elfu moja na wakubwa elfu mbili. Watu wote mnakaribishwa.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: