Wednesday, September 5, 2018

"Taifa Stars" kusafiri kesho saa saba kwenda kuwavaa Uganda Jumamosi


Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" inatarajia kufunga safari Kesho Alhamis Septemba 6,2018 saa 7 mchana tayari kuwafuata Uganda kwa ajili ya mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza Afcon mwakani. 

Timu hiyo itasafiri na kikosi cha wachezaji 23 na viongozi 7 watakaoambatana na viongozi mbalimbali wa TFF.

WACHEZAJI WATAKAO SAFIRI HIYO KESHO HAWA HAPA

Aishi Manula (Simba)
Beno Kakolanya (Young Africans)
Andrew Vicent (Young Africans )
Salum Kimenya(Tz Prisons)
Himid Mao (Petrojet,Misri)
Mudathir Yahya (Azam FC)

Mohamed Abdulrahiman (JKT Tanzania )
Hassan Kessy (Nkana,Zambia)
Gadiel Michael (Young Africans)
Abdi Banda (Baroka,Afrika Kusini)
Aggrey Morris (Azam FC)
Frank Domayo(Azam FC)

Salum Kihimbwa(Mtibwa),
Kelvin Sabato(Mtibwa)
David Mwantika(Azam FC) 
Ally Abdulkarim(Lipuli)
Simon Msuva (Al Jadida,Morocco)

Rashid Mandawa (BDF,Botswana)
Farid Mussa (Tenerife,Hispania)
Mbwana Samatta (KRC Genk,Belgium)
Thomas Ulimwengu (Al Hilal,Sudan)
Shabani Chilunda (Tenerife,Hispania)
Yahya Zaydi (Azam FC)

VIONGOZI

Kocha Mkuu Emmanuel Amunike na wasaidizi wake Hemed Morocco na Emeka Amadi,Mtunza Vifaa Ally Ruvu na madaktari wawili Richard Yomba na Gilbert Kigadya. 


Kocha Mkuu wa kikosi hiko Emmanuel Amunike anasema anaendelea na maandalizi akiendelea kuangalia mapungufu mbalimbali na kuyafanyia kazi ambapo anaamini kikosi kilichopo huku wachezaji wanaocheza nje wakiwa wameripoti wote. 

SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: