Tuesday, September 4, 2018

TAARIFA| Fahamu aina mbalimbali za wanaume waliyopo duniani,chagua aina inayokufaa mwanamke.


Pamoja na kwamba wanamme ndio wanatajwa kuwa walinzi wa familia na watafutaji wa kipato na chakula kwa familia, imekuja kubainika kuna aina nne ya wanamme hapa dunia. Aina hizo nne zimetokana na tabia mbalimbali ambazo zimejitokeza kwa wanamme waliopo hapa duniani.

Aina ya Kwanza- Wanaume Watoto (Childish Habit Men) hawa ni wanaume wasiokua kabisa. wana tabia za kitoto hapa kama wana umri mkubwa, wana matendo ya kitoto na siku zote wanawaza kama bado watoto na akiwa na mke au mchumba wanaweza wasifikie malengo tarajiwa.

Aina ya Pili- Wanaume Waliochanganywa na Mambo Mengi (Confused Men) Hawa ni wanaume walio na mambo mengi na mengi kati ya mambo hayo huwa yanawachanganya sana. Ukiwa na mme au mchumba mwenye tabia hii unabidi utumie akili nyingi kuwabadilisha.

Aina ya Tatu- Wanaume Wachezeaji (Player Men) Hawa ni wanamme waharibifu wasiokuwa na lengo jema kwenye mahusiano na hawana nafasi ya kujenga kitu hadi kikakamilika. Wengi wao wanakuwa na sababu mbalimbali katika kufanya uharibufu ila akielekezwa anaweza kubadilika au kutokubadilika.

Aina ya Nne- Wanaume wa Ndoto zako ( Right and Good Men) Hawa ni wanamme wenye ndoto njema kwa familia na watu wanaomzunguka. Pia kwenye mahusiano wako vizuri sio wahabirifu na wanajua kujituma kwa ajili ya watu wake wote. 

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: