Saturday, September 1, 2018

Raundi ya tatu ligi kuu yakamilika katika viwanja mbalimbali nchini.

Fabian Fanuel @FMG
MWANZA
Ligi kuu Tanzania Bara mzunguko wa tatu imeendelea leo katika viwanja mbalimbali huku timu zingine zikicheka na zingine zikilia kutokana na matokeo yaliyopatikana viwanjani.

Timu mpya kwenye ligi hiyo kutoka Mkoani Mwanza Alliance Fc walala mbele kikosi cha wajelajela Prisons kutoka Mbeya katika uwanja wa Sokoine kwa kufungwa goli 2-1 huku timu nyingi kwenye ligi Biashara kutoka Musoma Mara nayo ikilala kwa goli 1-0 ikifungwa na Stand United katika uwanja wa Kambarage Shinyanga.

Katika mashamba ya miwa Turiani Morogoro timu ya Mtibwa Sugar imeibuka mshindi didhi ya timu ngumu yaMbeya City kwa kuifunga goli 2-1 huku timu ya Kagera Sugar ikitoka sare didhi ya African Lyon katika uwanja wa Kaitaba.  Coastal Union nayo ikagawana pointi moja kwa moja didhi ya KMC katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: