Monday, September 3, 2018

NGOMA yuko fiti saana kujiunga na timu ni daktari tu kuamua arejee uwanjaniMshambuliaji mpya wa Azam FC, Donald Ngoma anatarajia kuanza kucheza mechi za ushindani baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua.
Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga raia wa Zimbabwe alikaa nje ya uwanja muda mrefu msimu uliopita akiwa na timu yake ya zamani ya Yanga kutokana na kuuguza goti.
Baada ya kusajiliwa Azam, Ngoma alipelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kupata matibabu ambapo sasa amepona na muda wowote kuanzia sasa ataanza kuonekana uwanjani.
Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd ameiambia Simba Makini kuwa wanasubiri ruhusu kutoka kwa daktari wa timu kuruhusu kuanza kucheza kwakua tayari amepona.
“Mchezaji Yakub Mohamed na Donald ngoma Wanaendelea vizuri saana tunasubiri tu go ahead ya daktari wetu kuweza kuwaruhusu warejee uwanjani,” alisema Jaffarry Iddi Maganga.
Azam itacheza mechi ya kirafiki kesho saa 12 jioni dhidi ya Arusha United katika mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex.
SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: