Wednesday, September 5, 2018

Neymar aipa ubingwa Man City Liverpool Arsenal hazitosa hazitashiriki ligi ya mabingwa
Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar Junior ambaye anakipiga kule nchini Ufaransa katika Klabu  ya Paris Saint Germany maarufu kama ``PSG`` Ametabiri msimamo wa ligi pendwa ya uingereza utakavyokuwa msimu utakavyo malizika.

Katika utabiri wake Neymar Amesema Manchester City itatetea ubingwa wake huku akiwapa nafasi ya pili klabu ya kutokea huko huko katika jiji la Manchester klabu ya Man United kumaliza  katika nafasi ya pili.

Nafasi ya tatu kwa mujibu wa utabiri wake ni klabu ya Chelsea the blues huku top four ikifungwa na Tottenham Hot Spurs.

Vilabu vya Liverpool na Arsenal havijapewa nafasi za kushika nafasi nne za juu na mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona Neymar Junior.

Hadi sasa Liverpool wanaongoza ligi ya Uingereza na alama 12 wakifuatiwa Chelsea yenye alama 12 kisha Watford katika nafasi ya tatu na alama 12 pia  huku man city ikiwa ya nne Tottenham ya 5 na united ya 10 zote zikicheza michezo 4 hadi sasa.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: