Friday, September 14, 2018

Mwimbaji wa Muziki wa Gospel Tumaini Lawi kuachia wimbo mpya kesho Youtube.

Sarah John @FMG
MWANZA

MWIMBAJI mahiri anayekuja vizuri katika muziki wa Injili Tanzania akitokea Mkoani Mwanza Tumaini Lawi anatarajia kuachia wimbo wake mpya ambao ulikuwa unasubiriwa kwa muda mrefu kesho jumapili.

Akizungumza na Famara News Tumaini alisema ameamua kufanya hivyo baada ya kuombwa sana na watu mbalimbali pamoja na baadhi ya mashabiki huo wimbo ambao wamepata nafasi ya kuusikia.

Tumaini alisema kuwa kutokana na uhitaji wa watu wa mahitaji wa walaji ameamua kuwapa zawadi mashabiki wake wote na anaamini wimbo huo utaleta mapinduzi makubwa na kuongeza chachu za kujituma kwa waimbaji waliomtangulia maana ameamua kuja tofauti na wengine.

Wimbo huo unaoitwa Hatutaachana utachiliwa kesho Jumapili Youtube na kusambazwa katika Radios na Mitandao yote ya kijamii kurahisisha watu waweze kuupata kirahisi ili kufaidi ujumbe uliomo ndani.

Sambamba na hilo Tumaini anapatikana kwa huduma popote pale maadam yawepo mawasiliano ya kati ya walengwa na yeye ili kwenda kusukuma kazi ya Mungu isonge mbele zaidi.

Anapatikana kwa namba +255 754 018 206 pia namba hiyo ndio yatumika Whatsapp. Youtube anatumia jina la TUMAINI LAWI. 

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: