Sunday, September 2, 2018

Mwimbaji Esther Tindos Kusekwa atamani kufika mbali kihuduma- Famara Media Group

Fabian Fanuel @FMG
MWANZA.

Mwimbaji wa nyimbo za injili na kijamii ambaye pia ni mtangazaji na mwandishi wa habari kutoka Living Water Fm Radio Mwanza Esther Tindo Kusekwa amesema kuwa anatamani kufika mbali kuhuduma katika kuelimisha kuburudisha na kuhabarisha.

Akizungumza na Mtandao wa Famara News Esther alisema kuwa anaamini Mungu amempa kipawa cha kuimba na amekuwa akifanya hivyo toka akiwa mdogo hadi sasa, kitendo ambacho kimempa kufahamiana na watu wengi nchini na nje ya nchi.

Esther ambaye kwa sasa amepata shavu la kuimba katika mwendelezo wa ukimbizwaji wa mwenge wa uhuru, akipata nafasi ya kuimba mkoa wa Simuyu, Mwanza na akitarajia kwenda pia mkoani Mara, mkoa ambao Mwenge utahamia baada ya kumaliza mkoani kuzindua miradi mbalimbali mkoani Mwanza.

Ameongeza kuwa kutokana na bidii, juhudi na kurekodi nyimbo nzuri ambazo zimekuwa zikipendwa sana na mashabiki hali iliyopelekea kupata mialiko mingi kwa sasa. 

Esther amesharekodi albam mbili za video za nyimbo za Injili nakuzifanyia uzinduzi katika jiji la Mwanza, na sasa amegeukia kuimba nyimbo za kijamii akirekodi wimbo unaitwa Magufuli ni Jembe ambao umetokea kukubalika kwa wadau mbalimbali hapa nchini kutokana na maudhi yaliyomo.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: