Sunday, September 2, 2018

Mwigulu Nchemba awapa nguvu na moyo waimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania- Famara Media Group.

Mwandishi Wetu @FMG
Morogoro.

Mbunge wa Iramba Mashariki Mwigulu Lameck Nchemba leo amewaongoza maelfu wa wananchi mkoani Morogoro katika tamasha kubwa ambali limeambatana na uzinduzi wa albam ya mwimbaji Tumaini Njole Sehaba uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.

Mwigulu ambaye ameambatana na wageni wengine akiwemo mbunge wa Ulyankulu John Kadutu, wachungaji, maaskofu kutoka madhehebu mbalimbali mkoani Morogoro.

Katika tamasha hilo kubwa, watu mbalimbali wamejitokeza kuja kushiriki baraka hizo ambapo wamepata upako wa nyimbo kutoka kwa waimbaji mbalimbali kutoka mikoa tofauti nchini Tanzania.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza uwanjani hapo, Mgeni Rasmi Mwigulu Nchemba alisema anaunga mkono juhudi za waimbaji wanaomtukuza Mungu kupitia nyimbo na kusema ataendelea kusapoti huduma hiyo maana ni huduma ambayo inampa Mungu utukufu mkubwa.

Mwigulu Nchema amekuwa mmoja katika ya viongozi nguzo katika kusapoti kazi ya Mungu kupitia huduma mbalimbali za utumishi, na amekuwa akialikwa sana na waimbaji wengi kwenye matamasha ya uzinduzi na mara kwa mara amekuwa akifika na kusema neno la kuwatia moyo waimbaji pamoja na watumishi wa Mungu kuhusu huduma waliotwa kutumika.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: