Thursday, September 6, 2018

Mshambuliaji hatari wa ‘Taifa Stars’ haoifi chochote mechi ya kesho asema wako vizuri



Mshambuliaji wa Tanzania ‘Taifa Stars’ Kelvin Kongwe Sabato amesema hawana mashaka kuhusu mchezo wao wa kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ utakaopigwa kesho saa kumi jioni kule Kampala Uganda kunako dimba la Namboole.
Sabato ni miongoni mwa wachezaji 23 wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ waliotua kule Uganda kuiwakilisha Tanzania  kuelekea Uganda kwa ajili mchezo huo.
Mshambuliaji huyo Machachari anayechezea klabu ya  Mtibwa Sugar ya turiani mjini Morogoro ni mmoja wa wachezaji saba walioongezwa kwenye kikosi hicho kufuatia kuenguliwa wachezaji wa Simba na mmoja wa Yanga walioshindwa  kuripoti kambini kwa wakati uliotakiwa .
“Mchezo utakuwa mgumu lakini hatuna sababu ya kuhofia tumejipanga vizuri na tunatarajia kupata ushindi hata kama ugenini,” alisema Sabato.
Sabato amekuwa kwenye kiwango bora na ndio kinara wa ufungaji wa mabao katika kikosi hicho cha Wakata miwa hao wa Manungu Turiani.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: