Tuesday, September 4, 2018

Mnyama Simba kukipiga jumamosi hii mechi ya kirafikiKlabu ya soka ya Simba inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki jumamosi hii dhidi ya wababe kutoka Kenya AFC Leopards mtanange utakaopigwa katika dimba la Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo utakaofanyika saa kumi na mbili jioni na umepangwa kufanyika muda huo ili kuwapa nafasi mashabiki kufuatilia mchezo wa kufuzu fainali za Afrika kati ya timu ya taif ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Uganda ‘The Cranes’.
Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa klabu ya mnyama Simba, Hajji Manara amesema viingilio vya mchezo huo kuwa ni VIP A ni sh 15,000 VIP B na C sh 10,000 na mzunguko sh 5000.
Ili kuongeza ladha ya mtanange huo pia Manara ameongeza kuwa mashabiki wataitazama mechi ya Stars dhidi ya ‘The Cranes’ kupitia Screen kubwa iliyopo uwanjani hapo.
Ligi imesimama kupisha mechi za kimataifa za kufuzu fainali za Afrika na itarejea tena Septemba 15.
Baada ya mchezo wao dhidi ya lipuli kupigwa tarehe na Bodi ya ligi kupitia shirikisho la soka Tanzania TFF Simba itasafiri kwenda Mtwara kucheza na Ndanda FC kabla ya kuelekea jijini Mwanza kukipiga na Mbao FC.SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: