Monday, September 10, 2018

Meneja Simba apigwa Faini ya millioni 4, na kutojihusisha na soka mwaka mzima kwa sababu hii hapaKamati ya Maadili ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imemfungia meneja wa klabu ya Simba, Richard Robert kutojihusha na shughuli zote za soka ndani na nje ya nchi kwa mwaka mmoja na faini ya milioni nne kwa kuchelewesha wachezaji kujiunga na timu ya taifa.
Meneja Richard  Robert amekutwa na makosa mawili ambayo ni kushindwa kutii agizo la TFF la kuruhusu wachezaji wa Simba kujiunga na kambi ya timu ya taifa na la pili ni kuhujumu timu ya taifa ya Tanzania.
Hamidu Mbwezeleni ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya hiyo,  amesema awali katika kesi hiyo alikuwepo kaimu katibu mkuu Hamis Kisiwa lakini aliondolewa kutokana na kuonekana hakuhusika kwenye sakata hilo.
Mbwezeleni amesema siku ya tukio Kisiwa hakuwepo na hata alivyoulizwa Robert mwenyewe alikiri katibu huyo hakuwepo na yeye ndiye alipewa maagizo hayo.


Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa hata baada ya kuambiwa na Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ ahakikishe wachezaji wanaripoti kambini saa 12 asubuhi bado alikaidi na kutaka kuwapeleka saa 6 mchana kitu ambacho kimeonyesha alidhamiria kufanya hujuma hiyo.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa baada ya Robert kuulizwa juu ya sakata hilo alikiri kupokea barua ya TFF juu ya kuitwa kambini wachezaji hao lakini hakuwa na uhakika kama mechi yao ya Lipuli ambayo ilipangwa kufanyika Septemba mosi iliahirishwa kweli au la.
“Kamati ya maadili imemtoa Hamis Kisiwa kwakua haku husika katika kesi hii na imemfumgia Richard Robert kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi kwa mwaka mmoja na faini ya shilingi milioni nne baada ya kukutwa na makosa mawili.
“Makosa hayo ni kushindwa kutii agizo la TFF kuruhusu wachezaji kuripoti kambini na la pili ni kuhujumu timu ya taifa. Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 5(2), 6c na H za maadili ya TFF,” alisema Mbwezeleni.
SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: