Thursday, September 6, 2018

Matokeo ya mechi za kirafiki Ureno yaambulia sare bila Ronaldo matokeo mengine haya hapaMichezo takribani nane ya kirafiki imefanyika usiku wa jana kule barani ulaya huku mchezo uliotazamwa na wengi ni ule wa ureno dhidi ya kaimu bingwa wa kombe la Dunia 2018 timu ya Taifa ya Croatia.

Katika mchezo huo ambao Ureno waliingia dimbani bila ya  huduma ya nyota wake Cristiano Ronaldo ambaye ameomba kusalia Turin ITALIA kuzoea mazingira, Ureno imeambulia sare ya goli 1-1,goli la ureno likifungwa na PEPE dk 32  huku la Croatia likiwekwa kimyani na Ivan Perisic mapema dk ya 18.

Matokeo ya mechi nyingine za Kirafiki ulaya jana..

Uholanzi 2-1 Peru


Katika Mchezo huo wa Uholanzi ulikuwa mchezo wa mwisho kwa kiungo Wesley Sneijder kuitumikia timu yake ya Taifa  ambayo ameshaichezea michezo 134 akifunga magoli 31 na kusaidia mengine 31.

Austria 2-0 Sweden
Jordan 0-1 Lebanon

Bahrain 1-1 Philippines
Trinidad And Tobago 2-0 U.A.E

Uzbekistan 1-1 Syria
Kyrgyzstan 1-1 Palestine


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: