Thursday, September 6, 2018

Matawi matatu ya mashabiki wa YANGA yafunguliwa wanayanga wamtaka Manji Kilimanjaro
Mashabiki lia lia wa klabu ya Yanga kata ya NJORO wameitisha kikao kwa lengo la kufungua tawi la mashabiki wa timu hiyo mkoani Kilimanjaro huku wakihitaji Mwenyekiti wa Yanga kufika mkoani huko.

Katika kufanikisha hilo wanayanga hao wa Kata ya Njoro wamefanya uchaguzi wa viongozi jana ambapo wamepata mwenyekiti Juma Athumani Mussa, Katibu Athumani Rajabu Chadua na Helen Anthony ambaye amekuwa Katibu msaidizi na wajumbe wengine nane wa Tawi la Yanga Njoro.

Katika kikao hiko ambacho kilisimamiwa na Mwenyekiti wa Mashabiki wa Yanga mkoa wa Kilimanjarob Albert Nyoka ambaye aliongoza pia zoezi la kuichangia klabu ya Yanga amewahaidi wanachama hao kuwa lazima Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji afike Kilimanjaro kwa wanachama hao.

Baada ya kufunguliwa Tawi hilo la Yanga kata ya Njoro sasa mkoa wa Kilimanjaro unamatawi matatu ikiwa ni Pamoja na lile la Newland na tawi la tatu likiwa katika kijiji cha mikocheni ambapo Albert Nyoka anaelekea huko siku ya jumatano kukamilisha taratibu za kufungua tawi.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: