Tuesday, September 18, 2018

Ligi ya Mabingwa Liver ni moto,Barcelona mambo safi
Kikosi cha Liverpool chini ya kocha wao Jurgen Klopp jana kimeanza vizuri michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kuichapa Paris Saint-Germain magoli  3-2 katika mchezo wa Kundi C uliopigwa katika Uwanja wa Anfield usiku wa jana Jumanne.

Mabao ya Liverpool yamefungwa na Daniel Sturridge dakika ya 30 na James Milner kwa penalti dakika ya 36 kufuatia Georginio Wijnaldum kuchezewa rafu kabla ya lile la ushindi kufungwa na mshambuliaji wake, Mbrazil Roberto Firmino  dakika ya 90 akitokea  benchi na kuifungia timu hiyo bao la ushindi.

Mabao ya PSG yamefungwa na Thomas Meunier dakika ya 40 na Kylian Mbappe dakika ya 83 ya mchezo.

 Matokeo mengine mechi za jana haya hapa
SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: