Sunday, September 2, 2018

Kocha wa Prisons awakubali Alliance kwa soka safi
Licha ya klabu ya Tanzania  Prisons ya Mbeya   kufanikiwa kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Alliance Academy kocha wa Tanzania Prisons, Abdallah Mohammed ‘Bares’ amekiri kuwa kikosi cha Alliance kimecheza soka safi saana hapo jana.

Mchezo huo wa ligi kuu ya Tanzania Bara (TPL) Ulipigwa mkoani Mbeya katika uwanja wa Sokoine na Kabla ya mchezo huo Prisons ilikuwa imepoteza mechi mbili za kwanza dhidi ya Simba na Mtibwa Sugar zote za ugenini.
Kocha Bares amesema Alliance walicheza kwa maelewano mazuri na waliwapa upinzani mkubwa lakini waliwazidi uzoefu na kuwabugiza mabao hayo.
 “Alliance ni timu nzuri na inacheza kwa maelewano makubwa, walitupa upinzani mkubwa ingawa tuliwafunga kwa uzoefu wetu kwenye ligi,” alisema Baresi.
Matokeo ya mechi nyingine ya za ligi kuu Tanzania bara (TPL) zilizopigwa JANA.
Stand United 2-1 Biashara
Coastal Union 1-1 KMC
Mtibwa Sugar 2-1 Mbeya City
Kagera Sugar 0-0 African Lyon
Tanzania Prisons 2-0 Alliance


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: