Sunday, September 2, 2018

Kikosi cha Mnyama Simba kufanya uchaguzi mapema mwezi wa 11 mwaka huuKamati ya uchaguzi ya klabu ya Mnyama  Simba kupitia kwa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Boniface Lihamwike imetangaza tarehe rasmi ya uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika Novemba 3 mwaka huu.
Katika uchaguzi huo nafasi zitakazo shindaniwa ni nafasi sita, nafasi ya Mwenyekiti, mjumbe mmoja na wengine wanne ambao wataingia katika bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo ya Simba yenye maskani yake jijini Dar es salaam.
Lihamwike amesema sifa ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti lazima awe na shahada ya kwanza, mjumbe mmoja pia lazima awe na shahada huku wale wanne wakitakiwa wawe na elimu ya kidato cha nne.
Pamoja na hayo Lihamwike ametaja ada katika nafasi ya Mwenyekiti ni shilingi laki tano wakati nafasi za wajumbe ni shilingi laki tatu tu za kitanzania.
Mchakato wa uchaguzi utakuwa kama ifuatavyo:
Septemba  3-11 kuchukua fomu muda saa 3 asubuhi -saa 10 jioni.
Septemba 11-15 kurejesha fomu saa 3 asubuhi -saa 10 jioni
Septemba 16-18, Usaili muda saa 3-10 jioni
Eptemba 21-23 S, kuweka pingamizi.
Septemba  24-26 kupitia pingamizi.
Septemba  27-29 kusikiliza pingamizi
Oktoba mosi kutoa maamuzi ya pingamizi.
Oktoba 2 kutangaza majina ya yaliyokidhi vigezo kwa uchaguzi.
Oktoba 3 hadi Novemba 2, Kampeni.
Novemba 3 Uchaguzi mkuu.
Lihamwike ameongeza kuwa uchaguzi huo utafuata katiba mpya ya Simba ya mwaka 2018 na kufwata kanuni za uchaguzi wa TFF.SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: