Wednesday, September 5, 2018

Kamanda Mambosasa atoa onyo kali kwa wanamgambo wanaopiga RaiaJeshi la Polisi Kanda maalum limeonya mamlaka mbalimbali kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kupiga watu kwa sababu yoyote ile kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa ameyasema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari.

Agosti 31 ilisambaa video kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mgambo wakimpiga raia kwa marungu akidaiwa  kukataa kulipa faini ya kuzoa takataka ambayo ni sh. 50,000.

Mambosasa amesema kama waliofanya kitendo hicho ni mgambo walipaswa kumkamata mhalifu na kumfikisha katika vyombo vinavyotakiwa badala ya kujichukulia sheria mkononi.

“Nchi hii inafuata misingi ya sheria kilichofanyika ni uhalifu na kimeifedhehesha nchi, hivyo kitendo kilichofanyika hakikubaliki hata kidogo,”amesema Mambosasa.

Amesema mgambo hao tayari walikamatwa na kufunguliwa mashtaka hivyo wanastahili kufikishwa mahakamani kwa kitendo walichokifanya.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: