Saturday, September 15, 2018

Jela miaka mitano kwa kughushi Imei namba za Simu.

NA OSCAR MIHAYO, MWANZA
MAMLAKA ya  Mawasiliano Tanzania (TCRA)  imeishukuru Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi ya mkoani Mwanza kwa kutenda haki mara baada ya kumuhukumu mshitakiwa Isaya Lucas kwenda jera miaka mitano kwa kosa la kughushi IMEI namba za simu.
Kesi hiyo namba 135 cha sheria ya elektroniki na posta ya mwaka 2010 imetolewa hukumu jana na hakimu mkazi mfawidhi Rhoda Ngimilanga.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hukumu hiyo nje ya mahakama Johanes Karungura Kaimu Mkurugenzi wa sheria na Katibu wa bodi ya wakurugenzi TCRA, alisema mshitakiwa huyo alikamatwa jijini hapa akiwa anabadilisha namba tambulishi za simu (Internationa Mobile Equipment Identity) IMEI.
Karungura alisema alikamatwa akibadilisha Imei za simu aina ya Tecno Cx Air ikiwa na imei namba 357201081915202 na 357201081915210 na kuzibadili kwenda namba 357901081915207 na 357901081915215, ikiwa lengo ni kufisha waharifu.
Alisema ubadilishaji wa Imei hizo inaweza kuleta athari katika nchi na usalama wa anga kimtandao, ikiwa kitendo cha hukumu ya leo kitasaidia kukomesha vitendo vyote katika kipindi hiki ambacho nchi inapambana kukomesha uhalifu.
Aidha ametoa onyo kwa wamiliki wa mitandao yote nchini kwa endapo mmiliki atapatikana anasaidia ama kujihuisisha kwa kusaidia wanaaobadilisha namba tambulishi haitawaangalia usoni.
“Mamlaka ya mawasiliano iko makini na hatulali usiku na mchana na hatutovumilia mtu yoyote ambaye anavuruga usalama wa anga na anasababisha vitendo vya kuwafanya wananchi wasiwe salama,” alisema.
Aidha Karungura alimaliza kwa kusema kuwa wote watakaobainika watashugulikiwa katika namna ya kuwafanya wananchi wawe salama.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: