Friday, September 14, 2018

EPL-Tottenham na Liver hapatoshi,united,Arsenal,Chelsea dimbaniIle ligi pendwa duniani ya uingereza EPL Kesho jumamosi itaendelea kwa michezo saba kupigwa kunako viwanja mbali mbali.
Mchezo unaosubiriwa na wengi ni ule wa Tottenham Hotspurs dhidi ya Liverpool utakaopigwa mapema saa nane na nusu kwa saa za Afrika mashariki.
Katika mchezo huo utakaopigwa katika uwanja wa Wembley Nyota wawili wa Timu mwenyeji  Tottenham Hotspur kiungo Dele Alli na mlinda mlango Hugo Lloris wanatarajiwa kuukosa mchezo huo.
Meneja wa Spurs, Mauricio Pochettino amesema Alli alipata majeraha akiwa na timu ya taifa ya Uingereza katika mchezo dhidi ya Hispania wa michuano mipya ya Ulaya kwa timu za taifa.
Dele 22, anaweza kukosa pia mchezo wa ugenini wa ligi ya mabingwa Jumanne ijayo dhidi ya Inter Milan kutokana na majeraha hayo.
Kwa upande wa Lloris aliumia katika mchezo walioibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Manchester United ambapo ilimfanya pia kukosa mechi ya Watford na ile ya timu ya taifa ya Ufaransa wiki iliyopita.
Lloris alipigwa faini ya pauni 50,000 na kutoendesha gari kwa miezi 20 kufuatia kukutwa na kosa la kuendesha akiwa amelewa ambapo ataendelea kukaa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa.

RATIBA YA EPL JUMAMOSI SEPT 15
Saa nane na nusu mchana
Tottenham Hotspur vs Liverpool
Michezo ya saa kumi na moja kamili jioni
AFC Bournemouth vs Leicester  City
Chelsea vs Cardiff City
Huddersfield Town vs Crystal Palace
Man City vs Fulham
Newcastle  United vs Arsenal
Mchezo wa saa moja na nusu usiku
Watford vs Man United
SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: