Sunday, September 2, 2018

Ebenezer Family Band kuzindua albam yao mpya uwanja wa CCM Kirumba Jumapili 9 September 2018.


Fabian Fanuel @FMG
MWANZA

Ebenezer Family Band kutoka Kanisa la EAGT Kiloleli Mwanza Jumapili tarehe tisa septemba mwaka huu saa saba mchan watazindua albam yao ya video iitwayo TULIZA MAWIMBI ambayo ina nyimbo kumi kwa pamoja.

Akizungumza na Mtandao wa Famara News Mwenyekiti wa Band hiyo Perusi Ezekiel alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na wanaamini kuwa watafanya kitu kikubwa cha historia katika jiji la Mwanza na kuongeza ubunifu mkuu katika kazi ya Mungu.

Alisema kuwa wamezialika kwaya mbalimbali kutoka Mwanza na nje ya Mwanza, Waimbaji wengine wa nyimbo za Injili kutoka Dar na Mikoa mingine kuja kuongeza nguvu katika uzinduzi huo.

Perusi alisema kuwa Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya, Jamii, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisindikizwa na wageni wengine kutoka Mwanza na mikoa mingine.

Ameongeza kuwa watumishi wa Mungu kutoka madhehebu mbalimbali mkoani Mwanza watakuwepo wakiwaongoza waumini wao katika kusapoti tamasha hilo ambalo litambatana uzinduzi mkubwa.

Ametaja kiingilio kuwa wakubwa watatoa elfu mbili na watoto watatoa elfu moja pale mlangoni

Tafadhali angalia tangazo hapoo chinii...Ubarikiwe sanaaa.
.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: