Friday, August 17, 2018

Yanga yamaliza kambi Morogoro kurejea Dar kwa basi kuwakabili waarabuKuelekea mchezo wa Yanga SC dhidi ya U.S.M. Alger ya Algeria hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika Jumapili hii Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kikosi cha yanga kimemaliza kambi yake mjini Morogoro na sasa wapo vizuri kukabiliana na waarabu.


Hizi hapa picha za Wachezaji wa Yanga SC wakiwa mazoezini leo asubuhi mjini Morogoro kabla ya kupanda basi kurejea Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ya Algeria Jumapili Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam .


Mchezo huo wa Jumapili safu ya ushambuliaji ya Yanga itaongezewa nguvu na mshambuliaji mpya, Heritier Makambo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambaye amepatiwa leseni na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Kocha Mkongo wa Yanga, Mwinyi Zahera anatarajiwa kuwa kwenye benchi la timu kwa mara ya kwanza tangu aajiriwe miezi miwili iliyopita.

Katika mchezo huo wa kundi D kiingilio ni shilingi  elfu tatu kwa majukwaa ya mzunguko, wakati watakaoketi VIP B na C watalipa Sh.elfu saba huku VIP A itakuwa Sh.elfu kumi tu.
SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: