Wednesday, August 29, 2018

Yanga yakamilisha ratiba kwa kichapo nchini Rwanda


Kikosi cha watoto wa jangwani Yanga kimeambulia kichapo cha goli 1-0 katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya  Rayon Sports mchezo uliofanyika nchini Rwanda leo.

Katika mchezo huo uliopigwa katika  Uwanja wa Nyamirambo Rwanda goli la ushindi limefungwa na Bimenyimana dk ya 19 kipindi cha kwanza.

Mchezo huo ambao uwanja ulitawaliwa na maji  Yanga walicheza soka safi na kuonyesha uwezo mkubwa licha ya kufungwa goli hilo moja kwa sifuri.

Katika mchezo mwingine wa kundi D Gor Mahia imefungwa na USM Alger kwa mabao 2-1 leo.

Baada ya matokeo hayo timu za USM Alger na Rayon Sports zimesonga mbele katika hatua inayofuata.

KUNDI D
TIMU             ALAMA
USM Alger        11
Rayon Sports     9
Gor Mahia         8
Young Africans  4

SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: