Sunday, August 26, 2018

Wilaya ya Misungwi yaongoza mkakati wa kitaifa wa kutokomeza Ukatili.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya anaeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kwa kutekeleza vyema mpango mkakati wa kitaifa wa miaka mitano kuanzia 2017/22 wa kutokomeza Ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake.

Nkima alitoa pongezi hizo Agosti 21, 2018 wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni maalum ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Kata ya Idetemya Halmashauri ya Misungwi, inayotekelezwa na Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI.

Alisema Misungwi imekuwa Halmashauri ya kwanza nchini kutafsiri kwa vitendo mpango huo na kulishukuru shirika la KIVULINI kwa kushirikiana na Halmashauri hiyo kupambana na vitendo vya ukatili hatua itakayosaidia kuelekea kwenye maendeleo endelevu bila ukatili wa kijinsia.
Tazama makala maalum hapo chini
Katibu Mkuu Wizara ya Afya anaeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ukatili kwa watoto na wanawake katika Kata ya Idetemywa wilayani Misungwi
Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye uzinduzi huo
Tazama hapa chini BMG Online Tv

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: