Sunday, August 26, 2018

Watoto na Vijana zaidi ya 300 wanufaika na Shirika la Wote Sawa.

NA OSCAR MIHAYO,
MWANZA
SHIRIKA la Wote Sawa limefanikisha kuunganisha zaidi ya  watoto wafanyakazi wa Nyumbani 300 kutoka jijini hapa kwa kuunda umoja wa vikundi 29, kwa lengo la kuwashirikisha katika shughuli za ujasiliamali, kijamii na kiuchumi.
Shirika limefanikisha mpango huo kupitia mradi wake wa  ujengewaji wa uwezo wa kijamii na kiuchumi kwa watoto na vijana wafanyakazi wa nyumbani kupitia ufadhili wa Foundation  For Civil Society (FCS).
Akizungumza na Famara News Mratibu wa vikundi hivyo Bi. Jenifer Kato amesema, wameamua kuanzisha umoja wa vikundi hivyo ikiwa na lengo la kuwaunganisha na kuwapatia elimu juu ya ujasiliamali, haki na wajibu kwa waajiri wao pamoja na  umuhimu wakuwa na mikataba.
Bi.Jenifer asema toka waanzishe vikundi hivyo wamefanikiwa kuwasainisha waajiri na waajiriwa mikataba, kushiriki mafunzo ya elimu ya ususi , baadhi yao kujiajiri na kuajiriwa pamoja na kuboresha maslahi ya mishahara yao kutoka Sh. 40,000 hadi sh. 80,000 kwa mwezi.
“Kwanza tumefanikiwa kuwatambua na kuchagua baadhi yao kushiriki mafunzo ya ujasiliamlai na wao kuja kuwa barozi mzuri kwa wengine na kufanya elimu hii kupanuka na kuwafikia watu wengi zaidi,”.
Kwa upande wake Katibu wa kikundi cha Umoja kilichopo Kata ya Nyamagana Capripoint jijini hapa, Bi. Annastazia Lawi alisema maisha kabla ya wote sawa yalikuwa magumu sana kutokana na manyanyaso na magumu waliyokuwa wanapitia.
“Kiukweli wote sawa imebadilisha maisha yetu na kutofanya na sisi tuonekane ni watu wenye staha katika jamii kwani kwa sasa tunaheshimiwa tunalindwa na tunapatiwa fursa mbalimbali na niombe elimu hii ienee nchi nzima ili ndugu zetu wanaoendelea na manyayaso waweze nao kuishi vizuri.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kapripoint Idara ya Maji Bw. Jovin Luhinda amesema uwepo wa vikundi hivyo kwenye mitaa yao unatambuliwa kisheria  ikiwa na kulinda maslahi yao pamoja na kuzuia watoto waliochini ya umri wa (14) kuajiriwa kwa shughuli hizo.


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: