Saturday, August 25, 2018

Wachezaji Yanga wagoma tena watano hawataenda Rwanda wadai chaoBaada ya kufanya vizuri kwenye michezo miwili ya kimashindano na wengi wakiamini imerejea, Wachezaji wa tano wa Klabu ya Yanga wanadaiwa wataukosa mchezo wao wa marudiano dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda unaotarajiwa kuchezwa Jumatano ijayo nchini Rwanda wakidai hadi walipwe chao.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika kutoka katikan klabu hiyo yenye rekodi nzuri ya kutwaa ubingwa wa bara mara 27 wachezaji wa tano ambao hawajatajwa wamezira kuja mazoezini kisa stahiki zao.
Inaelezwa kuwa kocha wa Yanga hafurahishwi na kitendo hicho kwani mwisho wa siku wachezaji wanaweza kujiunga na timu kuelekea nchini Rwanda wakiwa hawana mazoezi.
“Wachezaji ambao hawajafika mazoezini ni watano lakini siwezi kuwataja majina mtawaona wenyewe siku ya mechi, hii si nzuri sana kwani inaweza kuleta athari pale watakapokubali kwenda Rwanda huku wakiwa hawana mazoezi,” kimeeleza chanzo hicho.
Amesema kutofika mazoezi wakati wanajua fika wanatakiwa kuwa sehemu ya  mchezo sio jambo zuri na wanapaswa kufahamu thamani yao katika kikosi hicho.
Wengine ambao hawatakuwepo katika mchezo huo ni Mrisho Ngasa, golikipa Mkongo Klaus Kindoki na Fei Toto ambao  usajili wao haukukamilika Caf.SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: