Thursday, August 30, 2018

Wababe wa vigogo Mbao FC kukipiga leo na Singida united ratiba kamili hii hapaBaada ya kushinda michezo miwili mfululizo ya ligi kuu Tanzania bara Kikosi cha Mbao FC Wababe wa vigogo hii leo wataumana na wakamua Alizeti Singida united pale mkoani Singida.
Mchezo huo wa tatu kwa timu zote utachezwa katika uwanja wa nyumbani wa Singida united uwanja wa Namfua.
Mbao ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo wa TPL inakumbukumbu nzuri katika michezo yake baada ya kuichapa Alliance 1-0 mechi ya kwanza kabla ya kufanikiwa kushinda 2-1 dhidi ya Stand United ya Shinyanga na kuondoka na pointi tatu.
Singida united walifungwa mechi ya kwanza goli 1-0 na Biashara united kabla ya kushinda mechi yao ya pili dhidi ya mwadui goli 1-0 .
Ratiba ya michezo mingine ni hapo kesho
Coastal Union vs KMC
Kagera sugar vs African LYON
Mtibwa sugar vs Mbeya city
Stand united vs Biashara Mara
TZ Prisons vs AllianceSHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: