Friday, August 24, 2018

Vitu Vitatu vya kutazama mwanzo wa Ligi kuu Tanzania 2018-2019.

A)UDHAMINI MKUU HAKUNA
B)MGAO WA WADHAMINI WENZA KUWA CHINI
C)MAPATO YOTE KUCHUKUA MWENYEJI

Na Jumanne-Eden Ally

Ligi kuu Tanzania bara imeanza rasmi kwa viwanja kadhaa kupata fursa ya kutoa jasho kupambania alama tatu,moja au kukosa kabisa. Ligi hii tokea ipate hadhi ya kuitwa ligi kuu kutoka ligi daraja la kwanza imepitia vipindi kadhaa vya mpito katika uwekezaji tokea mwishoni mwa mwaka 1999 kuja karne mpya 2000. 

 Ligi hii iliwahi kuwa na mdhamini TBL mwanzoni mwa miaka hiyo na udhamini kuja kukoma mara baada ya FAT( sasa TFF) kufanya mabadiliko ya kucheza ligi ndogo kisha kuongeza timu shiriki kutoka 12 kwenda 16. Kesi hii inafanana na kipindi hiki kwa ongezeko la kutoka timu 16 kwenda 20. Mojawapo inatofautiana sana kutoka aliekuwa mdhamini wa ligi hii Vodacom Tanzania kuwa amemaliza kandarasi yake ya miaka mitatu. Ingawa taarifa isiyo rasmi zinasema kutokana na ongezeko la timu ndio chanzo. 

Ligi hii inaanza huku kukiwa na udhamini mwenza wa benki ya KCB na kampuni yenye haki ya kuonyesha matangazo ya runinga ya UHAI media. Kiasi watakacho pokea kwa kila timu ni milion 170+ ambacho kinadhalia ni kiasi kidogo kwa timu kujiendesha kwa miezi 9 kwa kusafiri, malazi, huduma ya afya, maandalizi na kulipa mshahara. Swali linalobakia kwa wadau wa mpira ni jinsi ligi itakavyo kuwa na dhima ya ushindani!.

Je suala la udhamini ni pekee kwa TFF na bodi ya ligi !?
Bado jibu la wengi litabakia kwa wahusika wakuu ambao wao wanaendesha soka kama ilivyo kwa la liga huko Spain. Upande wa pili napo ni changamoto ya timu zenyewe kubweteka na kutotafuta wadhamini wao binafsi. Udhamini wa overall bado hautoshi hivyo timu kupitia watu wa idara zao za masoko au katibu mkuu wanatakiwa pia kufanya kazi hii. Nao ni Kundi la kulaumiwa kwa kukosa kuanda mipango ya kufanya biashara katika soka. Club license inasisitiza haya na yakisimamiwa moja kwa moja kutapunguza ubwetekaji wa kutochangamkia fursa. 

Ingawa kuna changamoto ya ushawishi kwa vilabu vingi hususani vichanga kwa kutokuwa na kundi kubwa la wakereketwa wa timu hizi. Mfano timu kama mwadui, African Lyon,ndanda na nyingine ndogo zinahushawishi gani wa kuvutia muwekezaji ikiwa vina idadi ndogo mno wa mashabiki na wanachama. Timu kama Azam FC licha kuwa na udhamini mnono bado kuna changamoto ya return kwa mdhamini kutokana na ufinyu wa fan base ila kutokana na uwekezaji wao wa ndani imekuwa chachu kwao. 

Ukija kwa timu kubwa za Simba na Yanga,licha ya kuwa na ututitili wa mashabiki na wanachama ila uendeshaji wao kwa miaka mingi umekuwa unategemea huruma ya wadau wao. Hivyo kile wanachotumika kinatoka nje ya vyanzo vya mapato yao kama inavyotakiwa na kanuni. Ingawa simba,mbeya city zimeenda katika mabadiliko tunayosubiri kuona mafanikio kwao. 

Ligi kuu kuchezwa itachezwa ila kipi tunakitarajia timu zikianza kuyumba kiuchumi!? Tutapata wachezaji bora au bora wachezaji !? Ingawa hii sio mara ya kwanza kwa ligi kutokuwa na title sponsor. TFF, bodi ya ligi na timu ni muda wa kutatua changamoto hii kwa kufanya kazi ya kujenga msingi na thamani ya soka nchini.

Soka ni biashara na kila biashara lazima iwe na mbinu kubwa ili kufanikiwa kwa walaji. Kukiwa hakuna title sponsor, mgao kuwa mdogo kuna ili la makusanyo ya mlangoni kuchukuliwa yote na timu mwenyeji kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa ligi na timu zitakuwa zinapokea 60%. Huku sehemu nyingine zikienda katika mgao wa maeneo husika yaliohusu mchezo mzima. 

Ticket sells, ni moja ya chanzo kikubwa nje ya udhamini mkuu, udhamini wa timu,udhamini wa vifaa vya michezo ( ila Tanzania ndio umeanza), udhamini wa mambo ya insurance za afya na kadharika. Hapa licha ya timu hizi kupewa nafasi hii ila bado attendance ipo chini sana. 

Mashabiki wengi wamekuwa wazito kuja viwanjani na upenda matukio ya viwanjani kuliko mchezo wenyewe. Ikiwa huku kunategemewa sana kwa ajili ya kuziba mapengo ya gharama za uendeshaji. 

Je tumetengeneza njia salama kwa kupata matokeo ya kupata watu wengi!? Ligi hii ina mvuto wa kupelekea watu kuwa wanakuja kwa wingi angalau kwa wastani hata watu elfu 10 kwa kila mchezo!? Timu hizi zina star men wa kuvutia watu viwanjani!? Ukifikiria hivi ndipo unajiuliza utapataje udhamini ukiwa binafsi timu haina wachezaji wenye mvuto kwa mashabiki! Utajaza vipi viwanja ili kupata kipato kizuri cha mgao ukiwa unakosa nguvu ya kukosa uwekezaji mzuri!? 

Hivyo changamoto ipo kubwa katika kuleta watu viwanjani kama wafanyavyo Simba, Yanga kwa angalau. Mfano ligi kuu ya Serie A alipoteza mvuto kuanzia katika uwekezaji wa haki za matangazo, timu na hata maudhirio kwa muda mrefu ila sasa kiasi ujio wa Ronaldo umeongeza chachu kiasi. 

Simba msimu uliopita iliingiza kiasi kisichozidi milion 300+ na ndio walikuwa wanaingiza watu wengi,huku Mbao fc ikiingiza kiasi kisichozidi milion 60+ kwa mwaka katika gate correction. Ukitazama kinachoingia na kinachotumika kuna tofauti kubwa sana,bado vilabu vina mzigo mkubwa sana kujiendesha kwa kulipa gharama mbalimbali kwa msimu mzima. Hivyo bado makusanyo ya mlangoni licha mwenyeji kuchukua yote ila muhitikio upo chini kwa watu kuja viwanjani.

Tushukuru kwa uwekezaji kiasi uliopo kama KBC, Uhai media, Sportpesa, GF , Jambo,Michelin, Cocacola na nyingine nyingi kwa kujaribu kufanya uwekezaji unatia nguvu kiasi. Kubwa ni kuamka na kutazama fursa zilizopo. 

Jumanne-eden Ally ni mwandishi/ mchambuzi kutoka Lake fm 102.5 Mwanza.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: