Monday, August 27, 2018

Vijana waaswa kushiriki shughuli za kuwaingizia kipato na sio kukaa vijiweni kulalamika.LUCY SANKA @FMG
MWANZA
Wito umetolewa kwa vijana  wote katika jiji la mwanza  kuinua maendeleo katika kushiriki  shughuli mbalimbali ili kujipatia kipato pasipo kulalamika.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa shirika la Youth Environmental Vision  Bw Jonathan Kasibu amesema kuwa vijana wanatakiwa kushiriki katika maendeleo na siyo kulalamika kwana vijana wengi wamekaa tu mitaani wakidai hawana ajira.

Aidha ameeleza kuwa shirika hilo linawatambua vijana kwasababu ni nguvu kazi ya taifa letu hivyo vijana wafanye kazi na kuanzisha biashara ili baadae iweze kuwasaidia katika kufikisha malengo yao nahiyo itapelekea kukua kwa tanzanania ya viwanda.

Hata hivyo serikali ikisaidiana na mashirika mbalimbali ya mikopo katika kuwasaidia vijana mikakati ya mikopo vijana watakuwa na nguvu ya kuanzisha miradi mbalimbali na hatimaye kukuza uchumi wao wenyewe na taifa kwa ujumla.


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: