Sunday, August 26, 2018

Alliance Fc wasema hawatafanya kosa mara ya pili, mechi didhi ya African Lyon Jumatatu CCM Kirumba.

Mwandishi Wetu
Mwanza
Uongozi wa timu ya soka ya Alliance fc ya jijini Mwanza,mapema hii Leo umetaja viingilio katika mchezo wao wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya African Lyon utakaopigwa jumatatu ya August 27 katika Dimba  la Ccm Kirumba Mwanza.

Akizungumza na Blogu hii Mkuu wa idara ya Habari na Mawasiliano wa timu hiyo Jackson Mwafulango alisema,viingilio katika mchezo huo vitakua ni 5000 kwa mashabiki watakaokua Jukwaa kuu huku Mzunguko ikiwa ni Tsh.3000 pamoja na 1500 kwa watoto.

Mwafulango ameweka wazi kuwa wameamua kuweka viingilio vya Chini ili kuwapa Fursa mashabiki wa timu hiyo kujaa kwa wingi katika Dimba la Ccm Kirumba ili kuinga mkono timu yao kuhakikisha inapata alama tatu katika mchezo huo.

Alliance fc iko katika nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa haijapata pointi yoyote baada ya kucheza mchezo mmoja na kupotez kwa bao  1-0 dhidi ya Mbao fc.

Msikilize Jackson Luka Mwafulango alichokisema hapa.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: