Thursday, August 23, 2018

VIDEO-Samata apiga Hat trick yake ya kwanza barani ulaya
Mshambualiaji wa timu ya Taifa ya Tanzania  Mbwana Samata amefunga mabao matatu ‘hat trick’ yake ya kwanza barani ulaya akiisaidia klabu yake ya KRC Genk kuibuka na ushindi wa 5-2 katika mchezo wa kufuzu michuano ya Europa dhidi ya Broendby IF ya Sweden.
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amekuwa kwenye kiwango bora tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi na amefunga magoli hayo dakika za 37, 55 na 70 na kuendelea kuwapa raha mashabiki wa timu yake na watanzania pia.
Mabao mengine ya Genk yalifungwa na Leandro Trossard aliyefunga mawili dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati na jingine dakika ya 90.
Mchezo wa marudiano baina ya timu hizi mbili unatarajiwa kupigwa Agost 30 ili kumpata anayekwenda kushiriki michuano ya Europa kule barani ulaya.
Samata anatarajia kuingoza Stars kama nahodha katika mchezo wa kufuzu michuano ya Afrika dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ Septemba 8 jijini Kampala na kikosi kilichotajwa hivi karibuni na kocha mpya wa stars Emmanuel Amunike.SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: