Friday, August 17, 2018

Uganda yapiga mtu 6 wenzao Kenya wakipiga wa kwake 9 jioni ya leo

Kikosi cha timu ya vijana cha Kenya chini ya umri wa miaka 17 kimeiangusha kipigo kitakatifu cha magoli 9-0 kikosi cha Djibouti katika mchezo wa kundi B jioni ya leo uwanja wa taifa katika  michuano ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.


Baada ya ushindi huo timu ya Kenya sasa inafikisha alama 6 ikiwa imecheza michezo miwili na kusalia nafasi ya pili katika kundi B linaloongozwa na Ethiopia ambao wameshinda michezo mitatu hadi sasa wakiwa na alama 9 kibindoni.

Katika Mchezo mwingine wa kundi hilo Sudani ya kusini nayo imekumbana na kichapo cha goli 6-1 dhidi ya Uganda na kuwa kichapo cha pili kwa timu ya Sudani ya kusini katika mashindano haya.
SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: