Thursday, August 23, 2018

UEFA kumtunza David Beckham kwa mchango wake katika mchezo wa soka.

Na Jumanne-Eden Ally @FMG

Hii ni safari ndefu ya mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England na nahodha David Beckham katika kutangaza mchezo wa soka ulimwenguni vilivyo. Beckham alifahamika zaidi kwa uwezo wa kupiga mpira ya adhabu ndogo, kona muluwa na krosi zenye kufika kwa wahusika bila kusahau pasi ndefu za kukata uwanja. Pia unaweza kumsema ndio shujaa wa wachezaji wa kisasa kwa kuwa balozi wa kufanya mpira biashara kwa kuingia katika showbiz ya image right sanjali na matangazo makubwa ya kibiashara.

Hii imepelekea hadi sasa kubakia kuwa miongoni kwa wa wanasoka wasiocheza tena ila wanapata dili kubwa za matangazo ya biashara kama Adidas. Leo hii wachezaji kama Ronaldo, Neymar, Messi wanakuwa matajiri kutoka na kuwa na mikataba mikubwa ya kibiashara na haki za taswira. Becks anakumbwa zaidi kwa mafanikio akiwa na Manchester United msimu wa 1998/99 wakitwaa vikombe vitatu( Treble's). 
Kutokana na mchango wake huu Rais wa Uefa, Ceferin ameamua kumtunuku tuzo ya President's Award kwa mchango wake wa ndani na nje ya uwanja kwa kutangaza soka vilivyo "every corner of the planet".

Beckham licha kucheza vilabu vya Manchester United( Preston North End kwa mkopo), pia alicheza La Galaxy(USA), Real Madrid(Spain), AC Milan(Italy) na Paris St-Germain(France) kwa miaka 20. Sasa anatarajia kuzindua timu yake huko Miami na itacheza msimu ujao katika ligi ya MLS ya USA/Canada na pia anamiliki akademi nchini England.

Nje ya soka,Beckham anajishughulisha na kazi za kijamii akiwa balozi wa UNICEF wa kujitolea. 

"Beckham ni alama ya kweli katika soka kwa kizazi chake ",Rais wa Uefa Aleksander Ceferin amelisema.

Washindi wa miaka iliopita wa tuzo hii ambao walitazamwa kutokana na mafanikio yao, uweledi wao na uwezo wa ubora binafsi waliokuwa nao katika jamii the ni pamoja na Johan Cruyff, Bobby Charlton, Franz Beckenbauer, Bobby Robson na Paolo Maldini.

Beckham mwenye umri wa miaka 43, alicheza michezo 115 ya kimataifa akiwa na timu ya England na kushinda mataji 19 kwa vilabu alivyocheza sambamba na mataji 10 ya ligi.

Huyu ndio David Joseph Beckham, aliekuwa na alama ya jezi namba 7 akiwa Manchester United na England kabla kuanza kutumia jezi namba 23 kutokana na mapenzi yake kwa bilionea MWANAMICHEZO kutoka USA, Michael Jordan.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: