Wednesday, August 29, 2018

TFF yawaondoa wachezaji wa Simba kwenye kikosi cha Taifa Stars.


Wachezaji Sita wa timu ya Simba SC wametemwa kwenye timu ya Taifa Stars kwa kilichosemwa kuwa ni utovu wa nidhamu na kutokuwa wazalendo kwa timu ya taifa.

Wadau mbalimbali wa soka cnhini wamepokea taarifa hiyo iliyotangazwa na Kocha Emmuel Aminike kwa mtazamo tofauti kuhusu suala hilo huku wengi wao wakiponda uamuzi huo kuwa haujafuata kanuni na vigezo vinavyoendesha soka la Tanzania.

Wachezaji waliondolewa ni Erasto Nyoni, Shiza Kichuya, Hassan Dilunga, John Bocco, Jonas Mkude na Shomari Kapombe huku akibakia Aishi Manula pekee yako. Na tayari TFF imeshaita wachezaji wengine kujaza nafasi hizo.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: