Saturday, August 18, 2018

Simba Yatwaa Ngao ya hisani mara ya pili Mfululizo

 Kikosi cha Mnyama Simba kimefanikiwa kutwaa Ngao ya Hisani baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1 katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Magoli ya washindi Simba yamefungwa na  Meddie Kagere dk 29 na Hassan Dilunga dk 45 kipindi cha kwanza huku Bao pekee la Mtibwa likifungwa kwa shuti kali nje kidogo ya eneo la 18  na mshambuliaji wao Kelvin Sabato.

Kwa matokeo hayo simba inakuwa bingwa wa michuano hiyo mara mbili mfululizo mara baada ya kuwafunga kwa penati 5-4 Watani wao Yanga mwaka jana badaa ya suluhu ya 0-0.


Mabingwa wa Ngao ya jamii toka mwaka 2001

2001 Yanga 2-1 Simba
2009 Mtibwa 1-0 Yanga
2010 Yanga 0-0 Simba (penati 3-1)
2011 Simba 2-0 Yanga
2012 Simba 3-2 Azam
2013 Yanga 1-0 Azam
2014 Yanga 3-0 Azam
2015 Azam 0-0 Yanga ( penati 7-8)
2016 Yanga 2-2 Azam (penati 4-5)
2017 Yanga 0-0 Simba (penati 4-5)

2018 Simba 2-1 Mtibwa SugarSHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: