Friday, August 24, 2018

Serengeti boys yaambulia kichapo michuano ya Kombe la Cecafa chini ya miaka 17Timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys imekubali kichapo cha magoli 3-1 kutoka kwa vijana wenzao wa  Uganda katika michuano ya Kombe la Cecafa chini ya miaka 17 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mabao ya Ushindi ya  Uganda yamefungwa na Abdulwahid Iddi, John Alou na la jingine likifungwa na Alphonce Msanda akajifunga huku lile la kufutia machozi la Serengeti Boys lilifungwa na Edson Mshirakandi aliyechonga kona moja kwa moja.

Kwa ushindi huo, Uganda watawavaa Ethiopia katika mechi ya fainali siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa huku Serengeti Boys wakisubiri kucheza kuwania mshindi wa tatu dhidi ya Rwanda waliofungwa kwa penalti 4-2 na Ethiopia baada ya sare ya 2-2 katika muda wa kawaida.

Mshindi wa mchezo wa Fainali baina ya Ethiopia dhidi ya Uganda atakata tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika hapa nchini mwakani.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: